Felisi wa Gerona

Mt. Felisi akiwahubiria wanawake wa Gerona, mchoro wa Jean de Bourgogne (1470-1536).

Felisi wa Gerona (alifariki Gerona, leo nchini Hispania, 31 Agosti 304) alikuwa Mkristo kutoka Scillium, Tunisia, aliyekwenda pamoja na shemasi Kukufas kuinjilisha eneo la Katalunya akauawa wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian wa Dola la Roma[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Agosti[2].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/65170
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy